​NEMC YAICHARAZA MUCE BAO MBILI KWA MOJA MASHINDANO YA SHIMUTA


Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imeiadhibu timu ya Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) bao mbili kwa moja katika mashindano ya michezo ya SHIMMUTA yanayoendelea katika viwanja vya Jamuhuri Mkoani Dodoma.

Katika mtanange huo uliodumu kwa takribani dakika 90,kwa mapumziko ya dk 45 za kwanza NEMC ilijipatia bao la kwanza kutoka kwa mwanamazingira machachari Bw.Fortunatusi Patriki kwa shuti kali iliyopenyeza lango la MUCE katika dakika ya tatu ya mchezo baada ya kumzunguka beki wa kati wa timu ya MUCE wakati bao la pili la ushindi lilipatikana dakika ya 10 kutoka kwa mhandisi Msafiri Laurent na kuiweka NEMC katika nafasi nzuri ya ushindi wa bao moja dhidi ya MUCE.

Nao MUCE katika kujitafuta dakika 22 walifanikiwa kupata bao la kufuta machozi kupitia mchezaji wao Mwinyi Ramadhani na kufanya mechi hiyo kumalizika kwa NEMC kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja.

Katika mchezo huo pia MUCE walipata penati ambayo haikuzaa matunda baada ya mchezaji wao kushindwa kutamba mbele ya golikipa Tajiri Kihemba.

NEMC wamemaliza michuano hiyo wakiwa nafasi ya tatu hatua ya makundi upande wa mpira wa miguu kwenye kundi lenye timu tano ambazo ni TPA, Ngorongoro, TTCL, MUCE na NEMC yenyewe