Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini

Kitengo hiki kinaongozwa na Meneja.

Lengo

Kuratibu uundaji wa mipango ya ushirika na kusimamia utekelezaji wake.

Majukumu

Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mipango ya bajeti ya Baraza.

Kuratibu utayarishaji wa ripoti za utendaji mara kwa mara

Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango na miradi ya Baraza

Kuandaa na kuripoti utekelezaji wa mkakati wa uhamasishaji wa rasilimali za kifedha

Kusimamia utayarishaji na uboreshaji wa hifadhidata ya vifaa, taasisi na malipo ya ada na tozo.

Kuhudhuria na kufuatilia mikutano ya mapitio ya matumizi ya fedha za Umma inayoitishwa na mamlaka zinazoidhinisha mara kwa mara na

Kuratibu Mambo ya Bunge kwa kushirikiana na Wizara mama.