Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
Kitengo cha TEHAMA & Takwimu kinaongozwa na Meneja.
Malengo ya Kitengo:
Kutoa ushauri na utaalam juu ya maendeleo na utumiaji wa teknolojia katika utoaji huduma bora na uchambuzi wa takwimu.
Shughuli za Kitengo:
- Kuendeleza na kuendesha Mfumo wa Habari ya Mazingira (CEIS) na kuwezesha upatikanaji wa taarifa na habari kwa Umma;
- Kukusanya, kuchambua na kutoa takwimu za mazingira kwa matumizi anuwai;
- Kutengeneza habari za kijiografia kwa kutumia GIS na Remote Sensing kwa matumizi mbali mbali;
- Kuendeleza na kutekeleza mkakati wa teknolojia ya habari na mawasiliano;
- Kuendeleza na kusimamia tovuti ya Baraza;
- Kuendeleza na kudhibiti mifumo ya data na kuhakikisha usalama wake;
- Kutengeneza, kutunza na kuhifadhi miundombinu ya mfumo wa TEHAMA na kuhakikisha ushirikiano wa kiteknolojia na Taasisi zingine za Serikali pamoja na wadau;
- Kutekeleza sera ya Serikali ya TEHAMA;
- Uangalizi wa data za Baraza; na
- Kusimamia Maktaba na huduma za kituo cha habari ya Baraza.
Habari na Matukio
Matukio
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15