Kitengo cha Ukaguzi wa ndani

Kitengo hiki kinaongozwa na Meneja

Lengo

Kutoa huduma za ushauri kwa Afisa Masuuli katika usimamizi mzuri wa rasilimali za Baraza.

Majukumu

Kuratibu, kusimamia na kuhakiki ukaguzi wa fedha, ukaguzi wa ufanisi, ukaguzi wa mfumo na ukaguzi wa thamani ya fedha

Kutumikia kama Katibu wa Kamati ya Usimamizi wa Ukaguzi

Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa upokeaji, uhifadhi na matumizi ya rasilimali zote za fedha za Baraza.

Kukagua na kutoa ripoti juu ya matumizi na taratibu za kifedha na uendeshaji

Kupitia na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu wa hatua za menejimenti katika kujibu ripoti za ukaguzi wa ndani, na usimamizi wa ushauri kuhusu utekelezaji au mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kufanya ukaguzi wa ufanisi katika tathmini ya miradi ya maendeleo

Kuwasiliana na wakaguzi wa nje juu ya ukaguzi wa kila mwaka na kuhakikisha kuwa ripoti za Wakaguzi wa Nje zinafuatwa na usimamizi na kutekelezwa.