Kanda ya Ziwa Victoria

ENEO LA KIUTAWALA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Ziwa Victoria, ofisi zake zipo Mkoa wa Mwanza kama inavyoonekana kwenye anuani iliyopo mwishoni. NEMC Kanda ya Ziwa inahudumia Mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Mara, Geita, Simiyu na Shinyanga

VITENGO NA KAZI ZAKE

lli kutimiza na kufanikisha malengo ya Baraza, NEMC kanda ya Ziwa inafanya kazi zake kupitia vitengo vinne (4) kama ifuatavyo;

 • 1.KITENGO CHA UTEKELEZAJI NA UZINGATIAJI WA SHERIA ZA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL COMPLIANCE AND ENFORCEMENT-ECE).

Kazi zinazofanyika katika kitengo hiki ni:

 • Kaguzi za Kimazingira na Uzingatiaji wa Sheria za Mazingira
 • Ushughulikiaji wa Mchakato wa kutoa vibali vya Taka Hatarishi
 • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko ya jamii juu ya uchafuzi wa mazingira; na
 • Ukusanyaji wa ada na Tozo za Mazingira.
 • 2.KITENGO CHA TATHIMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT-ESIA)

Kazi zinazofanyika katika Kitengo hiki ni:

 • Kuratibu na kusimamia mchakato mzima wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Ukaguzi wa Mazingira baada ya kukamilika kuwasilisha Makao Makuu ya Baraza
 • Kuweka kanzidata ya Miradi inayosajiliwa na Kanda
 • Kuweka kanzidata ya vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Ukaguzi wa Mazingira vilivyotoka Makao Makuu.
 • 3.KITENGO CHA USIMAMAIZI NA UTAFITI WA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL RESEARCH AND MANAGEMENT-ERM)

Kazi zinazofanyika katika Kitengo hiki ni:

 • Elimu na ufahamu wa Mazingira kwa Jamii;
 • Kuandaa bajeti na mpango kazi wa ofisi ya Kanda;
 • Kuandaa mafunzo, semina na warsha ya masuala ya Mazingira; na
 • Kuratibu ushiriki wa Kanda katika matukio ya Mazingira (Environmental Envents)
 • 4.KITENGO CHA UTAWALA

Kazi zinazofanyika katika kitengo hiki ni usimamizi wa rasilimali watu na rasilimali fedha kwa upande wa Kanda ya Mwanza tu.

ANUANI

PSSSF Front Wing, ghorofa la 6,

Kitalu. 17/1, 17/2 & 18

Barabara ya Kenyatta,

S. L. P 11045, Mwanza

TANZANIA.

Simu namba: 0712/ 0689 224330, +255282541679

Nukushi: +255 28 2541679

Barua pepe: nemcmwanza@nemc.or.tz

Tovuti: www.nemc.or.tz