Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma

Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano Kinaongozwa na Meneja

Malengo:

Kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na masuala yote yanayohusu NEMC na kujenga uelewa kwa Jamii kuhusu usimamizi, utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira. Aidha Kitengo hurahisisha mtiririko wa taarifa kwenda kwa Jamii na kupata mrejesho toka kwa Jamii.


Majukumu ya Kitengo

Kutoa ushauri wa kitaalamu katika fani ya habari, elimu na mawasiliano kwa umma kwa Idara, Vitengo na wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Kukuza taswira chanya ya Baraza kwa Jamii

Kujenga uelewa kwa umma juu ya masuala ya mazingira na majukumu na kazi za Baraza.

Kukusanya na Kusambaza taarifa za Baraza na masuala ya mazingira kwa umma

Kuendeleza, kupitia na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Baraza

Kuandaa vipindi vya kukuza uelewa wa mazingira na uhamasishaji kupitia vyombo vya habari.