Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
<
Ofisi ya NEMC Kanda za juu Kusini ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma karibu zaidi kwa wadau. Ofisi ya Kanda inajishughulisha na masuala ya kukuza uelewa wa hifadhi ya mazingira kwa wadau; kufanya utafiti na mipango ya mazingira; usimamizi wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake; kusajili miradi ya uwekezaji na kusimamia mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na ukaguzi wa Mazingira, kutoa ushauri kwa wadau wa mazingira kuhusiana na usimamamizi wa mazingira na mali ya asili pamoja na shughuli zingine kama inavyoagizwa kwenye Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Ofisi pia inapokea maombi ya ukusanyaji, hifadhi, usafirishaji na uteketezaji wa taka hatarishi kwa ajili ya hatua za utoaji wa vibali vinavyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya mazingira.
Eneo la Linalohudumiwa na Ofisi ya Kanda
Kanda ya Nyanda za juu Kusini inashughulikia Mikao minne ya Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe.
Mipaka ya Kanda
MOROGORO- Upande wa Mashariki
RUVUMA – Upande wa Kusini
DODOMA and SINGIDA- Upande wa kaskazini
RUKWA – upande wa Magharibi
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15